DAR ES SALAAM.
Aliyekuwa Mgombea wa Nafasi ya Mwenyekiti Ndani ya chama cha ADC Doyo Hassan Doyo na wanachama wenzeka zaidi ya 70 wameungana na kupinga mchakato mzima wa mkutano mkuu wa chama, uchaguzi na matokeo ya uchaguzi kwani wanadai uendeshaji wa mkutano huo ulivunja kanuni na katiba za ADC.
Mkutano mkuu wa Chama hicho ulifanyika Jumamosi ya wiki iliyopita ya Tarehe 29/06/2024 katika Hotel ya Lamada Jijini Dar es salaam.
"Haki ya rufaa itatolewa kwa mgombea pekee,mgombea atalazimika kutoa notice ndani ya saa 24 kwa katibu wa rufaa".
Rufani yao inalenga kupinga uendeshaji wa uchaguzi,matokeo,na utangazaji wa matokeo katika mkutano huo, pia wamesisitiza kuwa wamepinga mfumo mzima kwakuwa umevunja katiba ya chama.
Sababu nyingine zinazowafanya kupinga matokeo hayo wamezitaja kuwa ni pamoja na "mkutano mkuu wa taifa wa uchaguzi mkuu lazima uongozwe na Mwenyekiti wa muda wa mkutano na atachaguliwa na wajunbe wa mkutano huo ambapo atasimamia uchaguzi wa Mwenyekiti wa chama wa kudumu".
"Mwenyekiti wa muda alieongoza mkutano huo ni Hamad Rashid ambaye ni Mwenyekiti mstaafu wa ADC na hakuchaguliwa na wajumbe wa mkutano mkuu, na aliongoza Mkutano mzima wakati alipaswa kuongoza kipengele cha uchaguzi pekee na kumwachia Mwenyekiti aliyechaguliwa kuongoza mkutano huo katija vipengele vinavyofwata ambavyo ni kuchaguliwa kwa Makamu Mwenyekiti na wajumbe Huo ni uvunjifu wa kanunua na katiba ya Chama".
Ameongeza kuwa Kanuni zinataka Mwenyekiti wa Mteule kutangazwa mara baada ya uchaguzi lakini katika mkutano huo haikuwa hivyo alitangazwa mwishoni mwa mkutano na Mwenyekiti wa muda aliongoza Mkutano mpaka mwisho jambo ambalo ni kinyume na utaratibu wa ADC.
Aidha amebainisha kuwa idadi ya kura iliongezeka kutoka wajumbe 168 ambao ni halali na kufikia kura 200.
Majina yaliyopelekwa kwa msajili wa vyama vya siasa ya wajumbe hayakutumika kuhakiki wajumbe wa mkutano mkuu na badala yake wakatumika watu wengine kwaajili ya kufanya udanganyifu na kumpitisha mgombea wanaemtaka ambapo wajumbe waliojiandikisha siku hiyo ni 192 na kura zikafikia 200.
Pia amesema licha ya kukata rufaa wameamuandikia taarifa MAALUMU msajili wa vyama kuhusu hali ya mkutano mkuu ulivyokuwa.
"Mimi niliishatangaza wazi matokeo nitakayopata nitaridhika nayo,lakini sio kwa utaratibu huu uliofanyika". amesema Doyo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa vijana, amesema uchaguzi mkuu ulitawaliwa na nguvu za Mwenyekiti aliyemaliza muda wake, kwani walijitahidi kuhoji jinsi mkutano unavyoendeshwa na Mwenyekiti huyo alikuwa akitoa majibu yasiyoridhisha na alikuwa akizuia wajumbe kusema lolote.
"Sisi hatuna uchu wa madaraka lakini tunataka haki itendeke,wametuahidi kutupa vyeo mbalimbali ndani ya ADC lakini hatupo tayari kuchukua vyeo hivyo bila haki kutendeka".
Naye Mgombea wa Makamu Mwenyekiti Zanzibar amesema aliombwa agombee nafasi ya Makamu Mwenyekiti lakini baadae alipigiwa simu na Hamad Rashid ambaye alikuwa Mwenyekiti wa ADC na kumwambia asigombee nafasi hiyo tena.
Pia alizuiwa kuonana na wajumbe kwaajili ya kuomba kura, kamati ya kupiga kura haikuruhusu mawakala wa wagombea kushudia zoezi la upigaji kura.
Hakuna maoni: