WAZAZI WAHIMIZWA KUTOA ELIMU YA HEDHI KWA WATOTO.


DAR ES SALAAM.

JAMII imetakiwa kutochukulia suala la hedhi kwa watoto wa kike kama ugonjwa badala yake kulichukulia suala hilo kuwa Mabadiliko kwenye ukuaji.


Wito huo umetolewa leo Jijini Dar es salaam na Mwandishi wa kitabu cha Shangwe,Mariam Mbano,wakati wakitoa msaada wa kitabu cha shangwe pamoja na Taulo za kike kwenye Shule ya Sekondari ya Goba mpakani Jijini hapa.


Mbano amesema bado kwenye jami kunakosa uelewa juu ya hedhi na kupelekea walezi kutumia njia ya mbadala ikiwemo kinyesi cha ng'ombe.


"Hedhi sio siri watu wapewe elimu,iwapo jamii ikosa elimu itapelekea Binti kushindwa kupata elimu "Amesema Mbano.


Hata hivyo,Mbano amesema Elimu ya Hedhi iwe jumuishi yaani wanamake na wanaume wote kwa pamoja wapewe elimu kwa upana ili kuondokana changamoto anayekutana na binti aliyekuwa na elimu sahihi ya hedhi.


Akizungumzia kitabu cha Shangwe,Wakili Mbano,amesema kitabu cha shangwe amesema kitabu hicho kinazungumzia wa watu wanavyofika Rika Balehe wanavyokosa elimu ya hedhi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mam'z Relationship Hup,Mhandisi,Frorian Miho,amesema wameichagua shule ya Sekondari ya Goba Mpakani wiliyani Kinondoni watatoa elimu pamoja na msaada wa vitabu,taulo za kike,nguo za ndani kwa wanawafunzi hao.


Mhandisi Miho amesema shule hiyo wanahitaji elimu kuhusu hedhi salama ili iwasaidie kutambua hedhi sio ugonjwa.


Mhandisi Miho amewaomba wazazi wasiwe waoga kwenye kuwaelimisha watoto wa kike ikiwemo kuwaanda kisaikolojia ili wakikutana na hali hiyo isiwatie uoga.


Huku nao wanafunzi wa shule hiyo ,akiwemo Mwanaheri Mapunda wa kidato cha nne pamoja Betrice Emanuel,wametoa shukrani kwa taasisi hiyo kwa msaada waliotoa shuleni hapo na kubainisha walikuwa wanakumbana na chang'amoto husika.

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.