KONGAMANO LA UJASIRIAMALI LATOA ELIMU NA FURSA KWA WAJASIRIAMALI WA YOMBO VITUKA.

Published from Blogger Prime Android App

DAR ES SALAAM.

Kongamano la ujasiriamali lililoandaliwa na The Dreams Foundation Events kwa kushirikiana na taasisi ya Tanzania save the community initiative ( TASACI) limewafikia wajasiriamali zaidi ya 150 kutoka Yombo Vituka, ambapo walipata elimu muhimu kuhusu uwekezaji, usimamizi wa mitaji, na fursa za maendeleo kiuchumi. 


Kongamano hili lililenga kuwawezesha wajasiriamali kupata ujuzi wa kuboresha biashara zao, huku likitolewa Mada na wadau mbalimbali, akiwemo UTT-AMIS,NMB na wawezeshaji wengine.

Published from Blogger Prime Android App
Akizungumza wakati wkifungua kongamhilo la wajasiliamali Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) Wilaya ya Temeke, Bi.Lawama Mikidadi amewahasa wajasiriamali kutumia sehemu ya faida yao kwa kutunza mitaji na siyo kutumia fedha zote kwa matumizi yasiyokuwa na manufaa. 

Amesisitiza kuwa faida inapokuwa kubwa, inaweza kutengwa kwa ajili ya matumizi ya lazima,kuweka akiba na kufanya uwekezaji katika taasisi za kifedha.

"Faida ikishakuwa kubwa unaweza kuitenga ikawaa sehemu ya kutuia na familia yako,ikaea sehemu ya kushereheka na jamii yako".Amesema Lawama.

Published from Blogger Prime Android App
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Yombo Vituka, Flugence Lwiza, amempongeza muandaaji wa kongamano hilo na kuwataka wajasiriamali wa Yombo Vituka kutumia elimu waliyoipata kama kichocheo cha mabadiliko katika ufanyaji biashara zao. 

Lwiza amesisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya wanaume na wanawake katika masuala ya ujasiriamali, akieleza kuwa kongamano hili lilikuwa ni fursa nzuri kwa kila mmoja kupata maarifa muhimu.

Aidha ameongeza kuwa wajasiriamali wana uwezo wa kutumia maarifa hayo kuboresha biashara zao na kuleta mabadiliko chanya katika jamii. Alisema kuwa ni muhimu kwa maafisa wa benki na taasisi za kifedha kutumia orodha ya wahudhuriaji wa kongamano hili kuwafikia wajasiriamali wengine na kuwapa habari kuhusu fursa za uwekezaji.

Published from Blogger Prime Android App
Nae Mkurugenzi wa The Dreams Foundation Events, Bi Hadia Akida, amesema kuwa taasisi yake imeanzishwa kwa lengo la kuwasaidia wanawake, vijana, wazee na watu wenye uhitaji, ili kuwafikisha kiuchumi. Alieleza kuwa wanawafikia wananchi nyumba kwa nyumba, wakiwaelimisha kuhusu changamoto zao na kuwasikiliza ili kujua mahitaji yao.

Pia Ameishukuru taasisi ya TASACI kwa kushirikiana nao katika kutoa mafunzo kwa wajasiriamali.

Mkurugenzi wa Tasaci, Japhet Mswaki, aliongeza kuwa taasisi yao imekuwa ikishirikiana na wadau mbalimbali ili kuhakikisha kuwa wananchi wanapata elimu muhimu kuhusu masuala ya biashara na ujasiriamali. Alisisitiza kuwa wajasiriamali walikuwa pia na fursa ya kupata mitungi ya gesi, lakini aliwahimiza kutumia mbinu za kudhibiti gharama za kununua gesi kwa ufanisi.

Wakizungumza wakati wa kutoa mada wa wakati wa Kongamano hilo Afisa masoko na mahusiano kutoka UTT-Amis, Afisa wa UTT, alionyesha kuwa wajasiriamali wengi wanakumbwa na changamoto ya mitaji na kutapeliwa kupitia vikundi vya vikoba na upatu. Alisema kuwa kampuni ya UTT-Amis inatoa fursa salama za uwekezaji kwa mtu mmoja mmoja, vikundi na taasisi, ambapo mtu anaweza kujiunga bure na kuanza kuwekeza na mitaji ya kuanzia Tsh. 10,000. Alisisitiza kuwa wajasiriamali wanaweza kuchagua mifuko mbalimbali ya uwekezaji na kupata faida kila mwezi.

Afisa kutoka NMB Temeke Godlove Joseph amesema umuhimu wa kufungua akaunti za vikundi na taasisi kwa ajili ya usalama wa fedha za wanachama. Alisisitiza kuwa kupitia benki ya NMB, vikundi na taasisi wanaweza kufungua akaunti bure kabisa, hivyo kuwa na uhakika wa usalama wa fedha zao.

Kongamano hilo ni jukwaa muhimu la kutoa elimu na fursa kwa wajasiriamali wa Yombo Vituka, na linatarajiwa kuwa endelevu kila mwaka ili kuongeza ufanisi na maendeleo katika sekta ya ujasiriamali.

Published from Blogger Prime Android App

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.