TPDC WASAINI MKATABA WA UJENZI BOMBA,MAKAME ATAJA SIFA LUKUKI TAIFA KUPATA


Na Karol Vicent

Dar es salaam.

SHIRIKA la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC)linatarajia kutumia zaidi ya Bilioni 120 kwa ajili ya ujenzi wa Bomba la Gesi asilia kutoka Ntorya hadi Madimba mkoani Mtwara


Akizungumza na waandishi habari mapema leo jijini Dar es Salaam,wakati wa Utiaji saini baina TPDC kwenye ujenzi wa bomba hilo na Kampuni ya China ya CPP na CPTDC

 ,Mkurugenzi Mkuu TPDC ,Mussa Makame,amesema ujenzi unatarajia kukamilika ndani ya miezi kumi na mbili na unajengwa kwa fedha za ndani za shirika zinazotokana na mapato yake.


Amesema Bomba hilo litakalojengwa litakuwa na inchi 14 na uwezo wa kusafirisha gesi ya futi za ujazo milioni 140 kwa siku, kiwango hiko cha gesi kinauwezo wa kuzalisha umeme wa megawati 700.



"Mradi huu ni muhimu sana kwa Taifa,Mnazi Bay na Songosongo zimekuwa za muda mrefu, Songosongo imezalisha gesi kwa miaka 20, Mnazibay miaka 18 na kiwango cha gesi kimeshaanza kupungua hivyo tunahitaji vyanzo vipya,”amesema Makame.


Aidha,Makame amebainisha kuwa mradi huo utahusisha ujenzi wa Bomba, ambapo kazi hii itatekelezwa na TPDC na kazi ya uchimbaji wa visima itatekelezwa na Kampuni ya ARA Petroleum kazi ambayo itakamilika kwa miezi 12.

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.