Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Mheshimiwa Swahiba H. Mndeme, amewasilisha rasmi Hati za Utambulisho kwa Mtukufu Mfalme Carl XVI Gustaf wa Sweden katika hafla maalum iliyofanyika tarehe 22 Mei 2026, kwenye Kasri la Mfalme wa Sweden lililopo jijini Stockholm.
Hafla hiyo ya kidiplomasia ni ishara ya kutambuliwa rasmi kwa Balozi Swahiba kama Mwakilishi rasmi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Sweden.
Aidha, hatua hiyo inafungua ukurasa mpya wa kuendelea kuimarisha uhusiano wa muda mrefu, wa kirafiki na kidiplomasia kati ya Tanzania na Sweden.



Hakuna maoni: