Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Ellen Maduhu, amefanya mazungumzo na Balozi wa Jamhuri ya Urusi nchini, Mhe. Andrey Avetisyan, katika Ofisi Ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam tarehe 22 Mei 2026.
Mazungumzo hayo yamelenga kuimarisha ushirikiano wa kimkakati kati ya Tanzania na Urusi katika sekta mbalimbali, ikiwemo elimu, biashara, afya na uwekezaji, kwa lengo la kupanua fursa za maendeleo pamoja na kuendeleza uhusiano wa kidiplomasia na kiuchumi kwa manufaa ya mataifa yote mawili.







Hakuna maoni: