WAZIRI wa Viwanda naDk Nicolaus Shombe Biashara ,Judith Kapinga, amesema Serikali inaendelea kuunga mkono uwekezaji katika viwanda vya uzalishaji wa pembejeo za kilimo ili kuhakikisha Tanzania inakuwa kitovu cha uzalishaji wa mbolea bora, salama na rafiki kwa mazingira katika ukanda wa Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla.
Ametoa Kauli hiyo May 30 Kibaha Mkoani Pwani wakati akizungumza kwenye hafla ya utiaji saini wa hati mbili za makubaliano ya ushirikiano ambapo makubaliano ya kwanza ni kati ya Tanzania Biotech Products Limited (TBPL) na Tanzania Fertilizer Company (TFC) na ya pili ni kati ya TBPL na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI).
Waziri Kapinga sema hatua hiyo ni utekelezaji wa azma ya Serikali ya kuongeza tija ya kilimo kupitia matumizi ya teknolojia, sayansi na pembejeo bora zinazolinda afya ya udongo, mazingira na wananchi kwa ujumla.
Katika hatua nyingine, Waziri huyo amezitaka taasisi zote zilizoingia makubaliano hayo kuhakikisha yanatekelezwa kwa vitendo na kuleta matokeo chanya kwa taifa, akisisitiza kuwa Serikali itaendelea kutoa ushirikiano unaohitajika ili kufanikisha malengo yaliyokusudiwa.
Pia ameuelekeza uongozi wa kiwanda cha TBPL kuimarisha mikakati ya masoko na utangazaji wa bidhaa zake ili kuongeza mauzo na kutumia kikamilifu uwezo mkubwa wa uzalishaji uliopo.
Kwa upande wake Mkutugenzi Mtendaji Dk Nicolaus Shombe,kutoka Shirika la Maendeleo la Taifa, ameeleza kuwa Kiwanda cha TBPL kina uwezo wa kuzalisha kiasi kikubwa cha bidhaa za kibaolojia kwa mwaka, huku mitambo yake ikiwa na uwezo wa kuzalisha zaidi ya tana 10 za bidhaa mbalimbali.
Amesema Mbali na viuatilifu vya kudhibiti mbu, kiwanda hicho pia kinazalisha viuatilifu vya mazao pamoja na mbolea za kikaboni zinazosaidia uzalishaji wa mazao ya kilimo hai yaaani organic farming.

Hakuna maoni: