TIRDO IMEFANYA MAKUBWA UJENZI WA MAABA ZA UTAFITI - KAPINGA

SERIKALI imesema kupitia Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) imeendelea kuimarisha na kuboresha maabara kwa ajili ya utoaji huduma za kitafiti katika maendeleo ya viwanda.

Hayo yamebainishwa leo mapema jijini Dodoma na Waziri wa Viwanda na Biashara,Judithi Kapinga,wakati wa uwasilishaji wa Bajeti ya Viwanda na Biashara kwa mwaka 2026-2027.

Amesema Katika mwaka 2025/2026 maabara ya chakula ambayo ilipata ithibati mwaka 2025 iliboreshwa kwa kuongeza wigo wa huduma kutoka huduma tatu (3) hadi sita (6) na wigo wa bidhaa kutoka moja 29 (1) hadi nne (4). 

" Huduma na bidhaa hizo ni pamoja na vyakula vilivyotayari kwa matumizi; nyama na bidhaa zake; samaki na bidhaa zake; na sampuli za usufi wa nyuso (surface swabs)"

"Kuongezeka kwa wigo huo kunaimarisha uwezo wa maabara kutoa huduma jumuishi na za kuaminika zaidi na kupunguza utegemezi wa huduma kutoka nje"amesema Waziri Kapinga.

Hata hivyo,Waziri Kapinga amesema pia TIRDO inaendelea na jitihada za kuanzisha Maabara ya Nishati na Madini katika Mkoa wa Njombe ili kusogeza huduma karibu na maeneo yenye rasilimali na shughuli za uzalishaji.

Amesema Uamuzi huuunatokana na uwepo wa makaa ya mawe katika maeneo ya jirani kama Ludewa, Mbinga na Nyasa na kusaidia kuongezeka kwa

mahitaji ya huduma za upimaji na uthibitishaji wa ubora wa nishati.Ambapo Maabara hiyo itahudumia Kanda ya Nyanda za Juu

Kusini (Ruvuma, Mbeya na Rukwa) na hivyo kupunguzagharama na muda wa upatikanaji wa huduma.

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.