BASATA WAFANYA ZIARA YA KIKAZI MAKUMBUSHO YA TAIFA







Jana tarehe 5 Juni 2026, Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Bw. Edward Buganga, alitembelea Makumbusho ya Taifa la Tanzania jijini Dar es Salaam kwa ziara ya kikazi yenye lengo la kuimarisha ushirikiano kati ya taasisi hizo mbili.

Katika ziara hiyo, Bw. Buganga alipokelewa na Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa la Tanzania, Dkt. Noel Lwoga, pamoja na viongozi na maafisa kutoka pande zote mbili. Mazungumzo yao yalijikita katika kubadilishana uzoefu wa kiutendaji, kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma, na kuimarisha ushirikiano katika kuhifadhi, kuendeleza na kutangaza urithi wa utamaduni wa Tanzania.

Aidha, ziara hiyo ilitoa fursa kwa viongozi hao kujadili maeneo mbalimbali ya ushirikiano yatakayochangia maendeleo ya sekta ya sanaa, utamaduni na urithi wa taifa kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.

Kaimu Katibu Mtendaji huyo aliambatana na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ukuzaji na Maendeleo ya Sanaa, Bi. Lilian Shayo, pamoja na maafisa wengine kutoka BASATA.

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.