Buguruni Yaishukuru Meridianbet

Uongozi wa kata ya Buguruni, iliyopo wilaya ya Ilala, jijini Dar es Salaam, umetoa shukrani zake za dhati kwa kampuni ya ubashiri ya Meridianbet kwa moyo wao wa kujitolea na kugusa maisha ya baadhi ya kaya masikini zinazopatikana kwenye mtaa wa Malapa kupitia msaada wa vyakula na vifaa vya usafi. Kitendo hiki kimeleta faraja kubwa kwa wakazi wa mtaa huu na kuonyesha kuwa bado kuna taasisi zinazojali jamii kwa vitendo.

Msaada uliopokelewa umejumuisha mahitaji muhimu ya kila siku kama mchele, unga, mafuta ya kupikia, sukari, maharage, sabuni za kufulia pamoja na bidhaa nyingine zinazotumika kwenye matumizi ya kila siku. Msaada huu umekuja kusaidia kupunguza changamoto zinazozikabili baadhi ya familia zilizopo mtaa wa Malapa.

Tunatambua kuwa kaya hizi sio chakula pekee wanachokihitaji, wanahitaji kuonekana, kukumbukwa na kuthaminiwa ingawaje wanapitia changamoto hizi za kiuchumi kwa sasa. 

Kwa niaba ya wakazi wote wa mtaa wa Malapa ndani ya kata yetu ya Buguruni, tunamshukuru mwakilishi wa Meridianbet Nancy Ingram pamoja na timu nzima ya kampuni hiyo kwa kututembelea na kutumia muda wao pamoja nasi. Uwepo wao umeacha furaha kubwa mioyoni mwa wananchi na kaya mbalimbali kwa namna moja ama nyingine na umetupa nguvu ya kuendelea kupambana na hali ya maisha bila kukata tamaa.

Tunaziomba taasisi nyingine pamoja na wadau mbalimbali lakini pia na wale wanaohusika na miradi ya kijamii kuendelea kuiga moyo huu wa kusaidia watu wenye uhitaji. Kata ya Buguruni itaendelea kuwa wazi kushirikiana na watu pamoja na kampuni zenye nia ya kuleta mabadiliko chanya kwa wananchi wetu wanaopitia hali ngumu za kimaisha. Kwa mara nyingine tena, tunasema asanteni Meridianbet kwa kuwa sehemu ya furaha ya wanamalapa.

Kata ya Buguruni yaishukuru Meridianbet kwa kugusa maisha ya wakazi wa mtaa wa Malapa kwa kutoa msaada wa vyakula na vifaa vya usafi kwa wenye uhitaji. Jisajili mtandaoni, na kwa wale wa USSD na vitochi piga,

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.