Jana Ijumaa tarehe 12 Juni 2026, Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE Plc) limefanya Mkutano Mkuu wa 11 wa Mwaka wa Wanahisa (AGM). Mkutano huo umejadili na kupitisha maamuzi mbalimbali muhimu, ikiwemo kuidhinisha gawio la kawaida la TZS 69.00 kwa kila hisa kutokana na faida baada ya kodi zilizopatikana mwaka 2025.
Aidha, wanahisa wameidhinisha gawio maalum la TZS 77.21 kwa kila hisa, na kufanya jumla ya gawio lililoidhinishwa kufikia TZS 146.21 kwa kila hisa.
Uamuzi huu unaendelea kuonesha dhamira ya DSE Plc katika kuleta thamani kwa wanahisa wake pamoja na kukuza uwekezaji endelevu nchini.


Hakuna maoni: