Mwandishi wetu,
Mombasa.
Shirikisho la waandishi wa habari Katika Ukanda wa Afrika Mashariki (FEAJ) limekutana katika mkutano Maalum kwa mara ya kwanza tangu viongozi wake kuchaguliwa mwaka jana ili kuweka Mikakati ya kusaidia Tasnia ya habari ukanda huo.
Akifungua Mkutano huo, June 20,2026,.mjini Mombasa ,Rais wa FEAJ Erick Oduor amesema lengo la shirikisho hilo ni kuwaunganisha wanahabari kufanya kazi pamoja na kutatua changamoto zao.
Oduor amesema, changamoto za wanahabari katika Ukanda wa Afrika ya Mashariki kwa kiasi kikubwa zinafanana hivyo ni muhimu kuwa na Mkakati wa Kikanda kutatua changamoto hizo.
Amesema FEAJ inakusudia kuwa na miradi kadhaa ya Kikanda ili kuboresha Utendaji wa wanahabari katika maeneo mbali mbali na kuwa na ushirikiano katika kuandika habari zenye manufaa kwa wananchi.wa Ukanda wa Afrika Mashariki.
Akizungumza katika mkutano huo, Rais wa Shirikisho la wanahabari Afrika (FAJ) Omar Faruk Osman aliwataka waandishi katika Ukanda wa Afrika Mashariki kuwaunga mkono viongozi wa FEAJ.
Amesema kumekuwepo na vyama vingi vya waandishi lakini FAJ inashirikiana na FEAJ katika kusaidia sekta ya habari,Uhuru wa vyombo vya habari na usalama Kwa Wanahabari.
"Waungeni mkono viongozi wa FEAJ ili kuimarisha Tasnia ya habari katika Ukanda wetu wa Africa ya Mashariki na Sisi FAJ tutaendelea kuwaunga mkono"amesema
Akizungumza katika mkutano huo,Katibu Mkuu wa FEAJ Solange Ayanone
amesema wanakusudia FEAJ kuwa na program za kuimarisha vyama vya wanahabari ili kuwasaidia kukabiliana na changamoto zilizopo.
Mjumbe wa Bodi ya JOWUTA,Tausi Mbowe akizungumza katika mkutano huo alishauri FEAJ kuwa na utaratibu wa kufanya mkutano katika Nchi zote wanachama.
"Lakini pia katika mikutano Waandishi wapate fursa kutembelea vitu vya kipekee katika kila nchi ili kujifunza na kutangaza shirikisho "alisema
Viongozi ambao waliochaguliwa kuongoza shirikisho hilo kwa miaka mitano ni Rais Odour ambaye ni Mkuu wa Chama Cha Waandishi Kenya,(KUJ) Makamu wa Rais Patrick Oyet Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi Sudan Kusini na Katibu Solange Kutoka.Chama cha Waandishi Rwanda.
Wengine ni Wajumbe wa Kamati Kuu ambao ni Mussa Juma Mwenyekiti wa Chama Cha Wafanyakazi Katika Vyombo Vya Habari Tanzania(JOWUTA )na Promise Twinamukye kutoka Chama Cha Waandishi Wafanyakazi Nchini Uganda.
Kabla ya mkutano huo , Viongozi na wanachama wa FEAJ walikuwa katika warsha ya siku tatu ya kuwajengea uwezo kuhusiana na masuala wa wahamaji na kubaini fursa zilizopo, mkutano ambao ulifadhiliwa na Shirika la kimataifa la Kazi Duniani (ILO) na wadau wengine.
Warsha hiyo ya Kikanda ilishirikisha Viongozi wa Vyama Wanahabari kutoka Comoro, Jibuti, Ethiopia, Kenya, Rwanda, Sudan, Somalia, Sudan Kusini, Tanzania na Uganda.



Hakuna maoni: