TIMU KUTOKA OFISI YA WAZIRI MKUU YAFANYA MAZUNGUMZO NA KATIBU TAWALA MWANZA KUHUSU MASUALA YA USIMAMIZI WA MAAFA

 


Na, mwandishi wetu,

Mwanza.

Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa Mwanza Bw. Henry Mwaijega amekutana na kufanya mazungumzo timu ya Idara ya Usimamizi wa Maafa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu walipomtembelea ofisini kwake leo 04 Juni, 2026 Jijini Mwanza.

Timu hiyo ipo mkoani Mwanza kwa lengo la kuongoza mafunzo ya usimamizi wa maafa kwa Kamati za Usimamizi wa Maafa mkoa pamoja na wadau mbalimbali, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuimarisha utayari, uratibu na uwezo wa kukabiliana na majanga katika ngazi ya mkoa.

Pamoja na mafunzo hayo, wanatarajia kuzindua Kituo cha Operesheni na Mawasiliano ya Dharura cha mkoa wa mwanza tarehe 05 juni, 2026.

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.