Na Mwandishi Wetu,
Dodoma.
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imeendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu masuala mbalimbali ya hali ya hewa kupitia Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma kuanzia Juni 16 hadi 23, 2026.
Maadhimisho hayo yalifunguliwa rasmi Juni 17, 2026 na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete, na yanatarajiwa kufikia kilele chake Juni 23, 2026.
Kupitia banda la TMA, wananchi wanapata fursa ya kujifunza namna ya kutafsiri taarifa za hali ya hewa na kutumia taarifa hizo katika sekta mbalimbali zikiwemo kilimo, usafiri na uvuvi. Elimu hiyo inalenga kuongeza ufanisi katika shughuli za maendeleo pamoja na kusaidia jamii kufanya maamuzi sahihi yanayozingatia mabadiliko ya hali ya hewa.
TMA imewahimiza wananchi kutembelea banda lake ili kupata uelewa mpana kuhusu huduma za hali ya hewa na mchango wake katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
Kaulimbiu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma mwaka huu ni, “Kuchochea Uwajibikaji Jumuishi kwa Huduma Endelevu.”


Hakuna maoni: