TGDC: TANZANIA INA FURSA KUBWA ZA UWEKEZAJI WA NISHATI JADIDIFU



Na Mwandishi Wetu

KAMPUNI ya Undelezaji Jotoardhi Tanzania (TGDC), imewaita wawekezaji kuwekeza katika uzalisaji wa nishati jadidifu ya jotoardhi ambayo inapatikana kwa wingi nchini Tanzania kwa kufuata miongozo na taratibu zilizowekwa na serikali ya Tanzania.

Wito huo umetolewa leo na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano TGDC, Khadija Faru wakati akizunguma na mwandishi wa chombo hiki, katika Viwanja vya Maonesho vya Kimataifa ya Sabasaba Dar es Salaam (DITF).

Faru amesema TGDC inaendelea na hatua ya uchorongaji wa kisima cha kuhakiki rasilimali iliyopo katika mradi wake wa Ngozi, MkoaniMbeya ambapo tafiti zimeonesha kuna nishati ya jotoardhi.

Mkuu huyo ametumia maonesho hayo kuwaomba wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kuja kuwekeza katika eneo hilo muhimu kwa uchumi wa nchi.

Pia Mkuu huyo amewakaribisha wananchi na wawekezaji kutembelea banda la kampuni hiyo lililopo katika viwanja vya sabasaba.

"Tuna miradi mitano ya kimkakati ambayo ni Ngozi, Kiejo Mbaka iliyopo mkoani Mbeya, Songwe Mkoani Songwe, Luhoi -Pwani na Natron - Arusha, hivyo tunaomba wadau wa sekta hiyo waje kuwekeza ili lengo la kuzalisha umeme wa jotoardhi lifanikiwe kwa kushirikiana na Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan ambaye ndiye kinara namba moja wa nishati safi nchini," amesema.

Faru amesema utafiti uliofanyika umeonesha nishati jadidifu ya jotoardhi inapatikana kwenye maeneo 52 ya mikoa 16, hivyo wawekezaji wasiwe na wasiwasi.

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.